Habari

Mambo ya kujifunza kwenye mpira wa kikapu na ukayatumia kwenye maisha ya kawaida

Kuna vitu vingi unaweza kujifunza kuhusu maisha kutoka kwenye michezo mbalimbali. Na moja ya michezo ambayo inatumia kanuni nzuri za msingi zinazoendana na maisha halisi ni mpira wa kikapu. Wengi wanapenda kuita basketball. Kwenye mchezo wa mpira wa kikapu unafundisha umuhimu wa kudumisha uwiano kwenye maisha yetu ya kila siku.

008091_christina

  1. Jifunze na kushika mambo ya msingi kwenye mchezo wa kikapu.  Kabla haujaanza kucheza mpira wa kikapu unatakiwa kufundishwa mambo ya msingi, namna ya kucheza mchezo huo, namna ya kudunda, namna ya kukimbia na kumpasia mwenzako na vitu vingine vingi. Hivyo unatakiwa kupata ujuzi wa vitu vya msingi ili uweze kucheza mchezo huo.

Somo la kujifunza: Kwenye maisha tunatakiwa kujifunza mambo ya msingi, unahitaji kujua maisha ni nini na msingi wake uko wapi. Hivyo ujifunze namna mbalimbali ya kukabiliana na maisha yenyewe. Usiende kichwa kichwa.

  1. Unatakiwa kujiandaa kiakili na mwili pia. Kama ulivyo mchezo wowote huwezi kushinda kama hufanyi mazoezi, akili na mwili wako lazima uwe umejiaandaa. Unahitaji kuwa na uzito fulani au kiwango fulani ili uweze kucheza kwa ustadi. Akili yako inatakiwa kuwa inayofikiri chanya, kukubali na kutii kutoka kwa mkufunzi wako.

Somo la kujifunza: Unatakiwa kujiandaa kiakili na kimwili ili kukabiliana na maisha yako ya kila siku.

  1. Usiwe mchoyo na ushirikiane na watu wengine. Mchezo wa mpira wa kikapu ni mchezo ambao unahitaji ushirikiano wa hali ya juu. Ili muweze kushinda kila mchezaji lazima acheze nafasi yake vizuri. Kila mmoja lazima mtizamo wake uwe kwenye huo mchezo ili kufikia malengo ya ushindi.

Mchezaji mkubwa kama Michael Jordan hakuweza kushinda mpaka pale alipojua umuhimu wa kushirikiana na wenzake katika kuwaamini na kugawana huo mpira. Katika michezo ambayo walishinda na yeye kupata magoli mengi zaidi ni pale alipoweza kupata vikapu 63 yeye peke yake lakini timu yao ilishindwa na Boston Celtics. Aliweza kujifunza kwamba umaarufu wake haukusaidia timu kushinda kwa sababu ya uchoyo wake na kutaka yeye tu ndio anatakiwa kufunga.

Kwenye maisha hivyo hivyo: Kama tunaweza kugawana na wengine ndivyo tunavyoweza kushinda au kufanikiwa. Kugawana hapa haimaanishi kuchukua mali ya wengine ila inamaanisha kuunganisha nguvu ili kufikia mafanikio ya kitu fulani labda ni biashara au kilimo n.k.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents