Habari

Mamilioni ya watu watahitaji msaada wa chakula 2023

Umoja wa mataifa na washirika wake wameomba msaada wa dola bilioni 51.5 kwa ajili ya kusaidia watu kwa mahitaji muhimu mwaka ujao 2023.

Kiwango hicho cha msaada ndicho cha juu zaidi kuwahi kuombwa na umoja wa mataifa, huku idadi ya watu wanaohitaji msaada kote duniani ikiwa inaendelea kuongezeka.

Dola bilioni 51.5 ni ongezeko la asilimia 25 ikilinganishwa na kiasi cha msaada uliotolewa mwaka 2022 na ni mara 5 ya ombi la umoja wa mataifa mwongo mmoja uliopita.

Umoja wa mataifa unakadiria kwamba watu milioni 65 zaidi ya idadi ya sasa watahitaji msaada mwaka ujao.

Vita vinavyoendelea Ukraine na hali mbaya ya ukame ni miongoni mwa sababu zinazopelekea idadi kubwa ya watu kuhitaji msaada hasa wa mahitaji muhimu kama chakula.

Vita vya Ukraine vimetatiza usafirishaji wa chakula na karibu watu milioni 45 katika nchi 37 wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents