Michezo

Man U kumuacha Ibrahimovic, mbivu mbichi kujulikana leo

Klabu ya Manchester United huenda isimuongeze mkataba mpya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika Juni 30.

Ijumaa hii kwa mujibu wa mtandao wa Goal, Klabu hiyo inatarajiwa kutangaza wachezaji kadhaa ambao wanaachwa na klabu hiyo huku jina la mshambuliaji huyo likidaiwa kuwepo.

Zlatan mwenye miaka 35 alisaini mkataba wa mwaka mmoja na kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Lakini mpaka sasa hakuna mjadala wa mkataba mpya na jeraha la goti alilopata mwezi April katika mchezo wa kombe la Europa ligi huenda likaongeza chachu ya kutopewa mkabata mpya.

Mshambuliaji huyu amecheza michezo 46 msimu huu na kufunga magoli jumla ya magoli 28

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents