Burudani

Man Walter awashauri ma-producer wa muziki Bongo kuweka wazi bei zao

Mtayarishaji wa muziki kutoka Combination Sound, Man Walter amewataka ma-producer wa muziki Tanzania kuwa huru kuweka wazi bei zao za kurekodi nyimbo katika studio zao, huku yeye akikiri kuwa wasanii waliogopa baada ya kuweka wazi bei ambayo anatoza na kukanusha siyo mpya ila ilikuwa haitambuliki.

man-walter-1

Man Walter ameiambia Bongo5 kuwa bei ya milioni moja inaogopwa kure , kwani bei hiyo ilikuwa toka mwanzo na ilikuwa inatumia kwenye nyimbo ziliitaji ufundi mkubwa.

“Yani baada ya kuweka wazi bei zangu za studio wasanii wameona kama mwaka umebadilika, mambo mpya, bei zimekuwa mamilioni, mpaka watu wanaanza kuogopa, kwanza mimi sijabadilisha bei, bei yangu ni ile ile sema watu wengi hawajawahi kufahamu studio wanarekodi shilingi ngapi?, yani bei za studio zimeonekana kama hazijawa wazi, hata ukiulizia studio za wengine kwa haraka haraka huwezi kupata bei, ndo maana nikawataka producers tuwe pamoja na kuweka bei zetu wazi, kwa upande wangu bei sijabadilisha bei ni ile ile ambayo ndo hiyo milioni moja, kupitiwa wasanii wengi kama akina Jide, Christian Bella ni wasanii ambao wanaelewa bei yangu ipo vipi, na wakati mwingine huwa tunashirikishana kutokana na aina ya wimbo, ugumu wa wimbo na kuna vitu vinahitajika tunagawana baadhi ya gharama ili nisi-base upande mmoja, kwahiyo nilikuwa nataka niwaambie watanzania na wateja wangu, wasije wakajua kuanzia milioni mpaka sijui mamilioni mangapi ndo mtu anaweza kurekodi, bei ni zile zile kama ambavyo watu walishawahi kurekodi kwangu na pia wanakaribishwa hata wale ambao hawajawai kurekodi tutazungumza na kushauriana maswala ya bei baada ya kuona unataka kufanya nini kutokana na ugumu wa kazi yako, wasiogope wakati mwingine tunamsikiliza mtu kulingana na wimbo wake ulivyo, unaweza ukalipa kutokana na wimbo wako ulivyo,” alisema Man Walter.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents