Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

Mapungufu Show ya Alikiba Simba day, Zuchu alikuwa na ulazima wa kukosoa show ya Alikiba??

Kupitia kipindi cha RECAP & MANDO @el_mado_tz ameichambua Show ya Alikiba aliyoifanya siku ya Simba Day wikienndi hii na kutoa mtazamo wake akiwa kama mdau wa burudani nchini.

@el_mando_tz amaeeleza kuwa show ya Alikiba haikuwa nzuri saa wala haikuwa mbaya sana bali ilikuwa ya kawaida sana kama wanavyofanya wasanii wengi kwenye matamasha makubwa kama hay yanayoandaliwa na vilabu.

Mbali ya msanii kuingia na Helkopta au kupanda juu ya kamba huwa hakuna ubunifu mwingine ambao huwa unafanywa na wasanii wetu kuleta tofauti sio tu kwa Alikiba bali wasanii wote hata waliopafomu siku ya Mwananchi (Yanga day)

Alikiba alionekana kufanya vizuri kwa sababu ya mambo haya yafuatayo.

1.Kwa sababu Alikiba ni msanii mkubwa hivyo ukubwa wake ulibeba show badala ya ubunifu wake.

2. Watu wengi walitaka kuona Alikiba akiimba Simba day maana alijitangaza yeye shabiki wa Yanga hivyo mashabiki wa Simba walikuwa na lengo la kuwakandia Yanga

3. Nyimbo ya MNYAMA. Nyimbo ni nzuri na kila mmoja alikuwa na mzuka nayo hivyo ilileta vibe la kitofauti.

Zaidi ya hapo hakua kingine cha ziada zaidi ya kuimba nyimbo zakle kama kawaida kwenye show zake zote.

Kitendo cha Zuchu kukosea show ya Alikiba alitaka kuiaminisha jamii kuwa yeye alifanya show kali zaidi haliyakuwa pia ilikuwa ya kawaida zaidi ya kuinngia na kamba uwanjani kitu ambacho kilishafanywa na wasanii wegine nyuma.

Unahisi kulikuwa na ulazima Zuchu kukosoa show ya Alikiba??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents