Habari

Marekani wamalizana na Wanamgambo wa Taliban

Marekani na kundi la wanamgambo wa Taliban wametia saini makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza vita vya miaka 18 nchini Afghansitan na kuwezesha Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini humo.

Image result for US and Taliban

Wakati wa hafla ya kuyatia saini makubaliano hayo iliyofanyika mjini Doha, Qatar, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Mike Pompeo ametoa wito kwa Taliban kuheshimu ahadi ilizotoa ikiwa ni pamoja na kukomesha mahusiano yake na makundi ya itikadi kali.

Chini ya mkataba huo Marekani itaanza kuondoa wanajeshi wake kwa makubaliano ya Taliban kuzuia mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Afghanistan.

Kwa mujibu wa DW, Pindi kundi la Taliban litatimiza masharti ya mkataba huo Marekani itaondoa wanajeshi wake wote ndani ya muda wa miezi 14 inayokuja Kutiwa saini mkataba huo kunatimiza moja ya ahadi muhimu ya wakati wa uchaguzi iliyotolewa na rais Donald Trump ya kuindoa Marekani kutoka vita visivyokwisha ikiwemo nchini Afghanistan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents