Michezo

Mashindano ya ‘Kitambi Noma’ kufanyika jijini Arusha

Jumla ya Klabu 16 zimethibitisha kushiriki Michuano ya ‘Kitambi Noma’ itakayofanyika Jijini Arusha mwezi huu wa Aprili, 2022.

Mwenyekiti wa Kitambi Noma Sports Club, James Rugangila amesema kuwa mashindano hayo yanayoshirikisha klabu za ndani na nje ya nchi yanatarajiwa kuanza tarehe 15 na fukifikia tamati Aprili  17, 2022 wakati wa kipindi cha sikukuu za Pasaka.

Kitambi Noma ni mashindano yanayohusisha wachezaji wa mpira wa miguu  ‘veterani’ ambao enzi zao waliupiga mwingi lakini kutokana na umri kwenda na majukumu ya kimaisha wameachana na mchezo huo na hivyo kutumia bonanza hilo kamasehemu ya kuimarisha afya.

Miongoni mwa klabu hizo 16 zitakazoshiriki 10 zinatoka Tanzania na sita (6) ni za nje ya nchi, Kitambi Noma Club, Mwangaza Veterans, Police Veterans – Arusha, Succa Veterans, Kijichi Veterans, Mipango Veterans -Dar es Salaam, Paris Veterans, Chini ya Muti Veterans, Green Yard Veterans, Nairobi West Veterans -Kenya na Kigali Veterans.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents