Tragedy

Mastaa waungana na wananchi kulaani tukio la kigaidi nje ya kanisa katoliki Arusha

Mastaa wa fani mbalimbali nchini wameungana na wananchi wa Tanzania kulaani tukio la mlipuko nje ya kanisa katoliki jijini Arusha leo. Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa huku 42 wakiwa na hali mbaya kufuatia tukio hilo lililotokea mida ya ya saa tano asubuhi katika kanisa katoliki la Olasit nje kidogo ya mji wa Arusha.

Baadhi ya majeruhi
Baadhi ya majeruhi

Wengine kadhaa walijeruhiwa huku balozi wa papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya kuzindua parokia mpya ya mtakatifu Yosefu walinusurika.

Mmoja wa majeruhi akifikishwa hospitali
Mmoja wa majeruhi akifikishwa hospitali
Viatu vilivyobaki baada ya mlipuko
Viatu vilivyobaki baada ya mlipuko
Huduma ya kwanza
Huduma ya kwanza

Kwa mujibu wa RPC mkoa wa Arusha, tukio hilo ni la kigaidi na kwamba wanawasaka wote waliohusika na tukio hilo. Jeshi la polisi tayari linamshikilia mtu mmoja akihusishwa na mlipuko huo.
Mtu anayedai kutupa bomu hilo, anaaminika kutumia bomu la kutengeneza kwa petrol na kulitupa karibu na choo kilichopo karibu na mlango mkuu wa kanisa hilo.

Hizi ni baadhi ya tweets za mastaa hao:

Producer Mbezi

I Think samtin z not right_and sam1 z behind all thiz.I stil can’t belev km ni udini ndo tunalipuana.t must b sam1 among all this.POLEN waTz. Bado nahisi kama mtu anatumia kigezo cha udini kututeketeka.we have to stay strong and stick 2gthr.let’s not giv them chance.Tuitunze amani.

Jokate Mwegelo

Wapendwa viongozi wetu, kusema pole tu haisaidii. Tafuteni chanzo cha mlipuko, mtuambie pamoja na mikakati mtakayoweka kulinda wananchi. Uongozi sio masihara. Kama kuna mtu hana uchungu na hii nchi na wananchi hatufai kama kiongozi bora ukalime shamba tungojee mazao kiangazi.

Nick wa Pili

Ni muda wa kukaa kimia kutafakari na kuchunguza kwa kina sana…na kuhakikisha haki inatendeka….inasikittisha sana haya kutokea Tanzania.

Albert Mangwair

Wazungu na Waarabu kiboko wamekuja tufanya watumwa wamechukua kila kitu Maisha Magumu now tunapigania Dini zao mweeeh Maisha Magumu Jamani

Diva ‏

Thinking The day Christians watapokosa Uvumilivu in this country… Mapadre kuuwawa,makanisa kuchomwa moto&etc . Think The Government na vyombo vyake shuld find out nani hasa anafanya vitendo hivi kiukweli.Why churches Being Epicenter of the Attacks?

Rose Ndauka

Poleni sana Arusha kwa majanga haya, tuko pamoja watanzania tumeguswa na kitendo cha kikatili. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania

Solothang

Damn sikujua yaliyojiri Arusha ,, Daah inaskitisha na poleni waathirika ,,,,,, so sad. #UDINI ni #kirusi Hatari sana ,na ni S.U.M.U ambayo tukiinywa, tutaambukizana Chuki,Uhasama, tusipojikinga na kuelimishana ,Damu itamwagika! Nani kaleta #Udini Tanzania??? hatukuana matukio mfululizo kama haya miaka 10 ilyopita!!! wapi tunakwenda??

Kwa mujibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni paroko msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Arusha, mripuko ulipotokea walikuwa tayari kubariki maji kwa ajili ya uzinduzi wa kanisa, shughuli iliyokuwa ikiongozwa na balozi wa Papa Francis.

Hata hivyo Padre Mangwangi ameliambia shirika la habari la Uingereza, BBC kuwa taarifa walizonazo muda mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali, kuna watu watatu kati yao waliofariki na wengine wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru mjini Arusha.

Watalaalamu wa milipuko na polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo. Bado hakuna taarifa ya chanzo cha mripuko au kama kuna mtu au kundi lilohusika.

Hili ni shambulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japokuwa mwaka huu pia kulikuwa na tukio la mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani Zanzibar, ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia kanisani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents