FahamuHabari

Mfannyakazi akimkosoa Elon Musk hana kazi

SpaceX inashutumiwa kuwafukuza wafanyakazi nane kinyume na sheria kwa sababu walikuwa wanamkosoa bilionea Elon Musk.

Malalamiko hayo yameelezwa na taasisi ya ajira ya Marekani kuwa wafanyakazi walituma barua ya wazi kwa wakurugenzi wa taasisi mwaka 2022, wakielezea wasiwasi wao katika mahali pa kazi.

Barua hiyo ilimwelezea Musk kuwa ni “msumbufu na anaefedhesha,” kulingana na shirika la habari la Reuters.

Malalamiko ya afisa wa kikanda katika Bodi ya Kitaifa ya Mahusiano ya Kazi (NLRB) inaishutumu SpaceX kwa kukiuka haki za wafanyakazi chini ya sheria ya shirikisho la kazi ambalo linaruhusu wafanyakazi kwa pamoja kupambania mazingira bora ya kazi.

Malalamiko hayo pia yalisema waliohusika katika barua hiyo ya wazi walihojiwa kabla ya kuachishwa kazi.

Mawakili wa mmoja wa wafanyakazi wa zamani, Deborah Lawrence, wameripotiwa kuishutumu SpaceX kwa kuwa na “mazingira magumu,” ambapo unyanyasaji unavumiliwa.

Katika taarifa yake, iliyoonwa na Reuters, Bi Lawrence alisema: “Tuliandika barua ya wazi kwa uongozi sio kwa nia mbaya, lakini kwa sababu tuljali maslahi ya watu wanaotuzunguka.”

Ikiwa SpaceX haitatatua suala hili, kesi itasikilizwa na jaji wa utawala, ambaye uamuzi wake unaweza kuwapelekea kukata rufaa kwa bodi na kisha kwa mahakama ya rufaa ya shirikisho.

Kesi imepangwa kusikilizwa tarehe 5 Machi.

Hata hivyo sheria ya kazi, inaweza kuamuru wafanyakazi warejeshwe kazini na kulipwa mishahara.

Kampuni za Bw Musk zimeshutumiwa kwa kukiuka haki za wafanyakazi hapo awali.

Mwezi Oktoba, NLRB iliishutumu X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, kwa kumfukuza mfanyakazi kinyume cha sheria juu ya machapisho katika X (Twitter) ya kupinga sera ya kampuni ya kurudi ofisini.

Lakini X ilikanusha makosa hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents