Habari

Mgodi waua watu 52 wakiwemo waokoaji Siberia

By; Godfrey McDanniel Mgallah

Watu 52 wakiwemo waokoaji sita wanaaminika kufariki katika ajali iliyotokea kwenye mgodi wa makaa ya mawe wa Siberia.

Mgodi huo ulioko karibu na mji wa Belovo katika mkoa wa uchimbaji madini wa Kemerovo, ulionekana kujawa na moshi jana asubuhi, huku watu zaidi ya 200 wakiwa ndani.

Awali maafisa walisema kwamba wachimba migodi wengi walifanikiwa kutoka lakini 11 na waokoaji watatu walipoteza maisha, na wengine 35 hawajulikani waliko baada ya ajali hiyo. Zoezi la uokoaji lilisitishwa baada ya maafisa kudai kuwa kulikuwa na kitisho cha mlipuko.

Ajali za migodini zimekuwa zikitokea mara kwa mara nchini Urusi na katika eneo la zamani la Umoja wa Kisovieti kwa sababu ya viwango duni vya usalama, na ukosefu wa usimamizi wa mazingira ya kazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents