Burudani

Mkubwa Fella aja na Singo Yake

Mkubwa Fella ameingia studio ya Sound Crafterz kwa
ajili ya kurekodi singo yake ya kwanza itakayoitwa 2009. Amesema kuwa
anataka kuwaonesha baadhi wasanii ambao wamekuwa wakimfuata wakati wa
shida na kusaidiwa..

Anaitwa Said Fella lakini unaweza ukaanza kumuita kwa jila la Mkubwa
Fella nae bila hiyana huitika kwa bashasha kabisa. Kwa wale wasiomfahamu
vyema ni yule meneja wa kundi la Wanaume TMK Familly lenya makao yake
makuu kule kule Temeke jijini Dar.

Mkubwa Fella ameingia studio ya Sound Crafterz kwa
ajili ya kurekodi singo yake ya kwanza itakayoitwa 2009. Amesema kuwa
anataka kuwaonesha baadhi wasanii ambao wamekuwa wakimfuata wakati wa
shida na kusaidiwa, wakishiba wanakuja na maneno ya kashfa na kiburi
kama baadhi ya wasanii wengine ambao wamekuwa wakimtuhumu kwa maneno ya
hapa na pale.

“Nataka kuwaonesha baadhi wasanii kuwa hata mimi
na naweza,ili kuthibitisha hilo wakae mkao wa kula nakuja na singo
yangu ya kwanza itakayoitwa 2009, sasa nipo studio ya Sound Crafters
kwa ajili kurekodi hiyo singo,ambayo anaamini itawashtua wengi, kwamba
aalahh hata Mkubwa Fella anaweza” alibainisha Mkubwa Fella.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents