Stara kuwasha moto Bilicanas

Mwanamuziki mahiri wa miondoko ya zouk na taratibu ‘Rhythm &
Blues – R&B’, Stara Thomas Mbiti, amesema kwamba kwa sasa ameanza
kazi rasmi ya muziki baada ya kusimama kwa miaka takriban miwili.

MWANAMUZIKI mahiri wa miondoko ya zouk na taratibu ‘Rhythm &
Blues – R&B’, Stara Thomas Mbiti, amesema kwamba kwa sasa ameanza
kazi rasmi ya muziki baada ya kusimama kwa miaka takriban miwili.

 

Stara alisema hayo jijini Dar es Salaam, kwamba ataanza
kufanya onyesho Club Bilicans, ukumbi mkubwa wa burudani Afrika
Mashariki na Kati.

 

“Ndiyo, nina programu Jumatano (tarehe 28 Januari 2009) hapa Bilicanas,” alisema Stara
katika mahojiano ya papo kwa hapo mara baada ya kutembelea ofisi za
Tanzania Daima na Sayari jijini. “Nadhani itakuwa mfululizo,” aliongeza.

 

Akihojiwa sababu za kutokuwa hewani kwa kipindi kirefu, Stara alisema:
“Muziki si jambo la kukurupuka. Na isitoshe nilikuwa katika likizo ya
uzazi.”

 

Stara alipata mtoto wa pili, miaka miwili iliyopita na amempa jina la
Jazz, mdogo wa Nicole, ambaye alimzaa miaka takriban saba iliyopita.

 

Alipohojiwa sababu za kumwita mtoto huyo Jazz, alijibu: “Aaaah, ni kwa
sababu wakati nimebeba ujauzito huo, nilikuwa na nguvu wakati wote,”
alisema na kuongeza:

 “Can you imagine (unaweza ukafikiri) hata wakati nafanya wimbo wa
‘Wasiwasi wa Mapenzi’ nilikuwa tayari nimekamilisha miezi tisa, lakini
nikawa na nguvu za ajabu na sikuona ulegevu au dalili za kuchoka mpaka
nikajifungua, ndiyo maana mtoto nikamwita Jazz,” alisema mwanamuziki
huyo mwenye mapenzi na muziki wa jazz.

 

Huu ni ujio mpya wa msanii huyo ambaye amekwisha wahi kutamba na nyimbo
kadhaa ukiwamo ‘Mimi na Wewe’ na sasa ana kibao kipya kinachokwenda kwa
jina la ‘Nini Sina’ alichomshirikisha msanii Rashid Abdallah ‘Chid
Benz’.

 

Source: Tanzania Daima

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents