Burudani

Morgan Heritage watumia picha ya kampeni za CCM Mwanza kudai ni watu waliohudhuria show yao ya Nairobi

Kundi la reggae kutoka Jamaica linaloheshimika zaidi duniani, Morgan Heritage limeamua kwa kujua au kwa kutokujua kuudanganya umma!

Morgan-Heritage

Kupitia Facebook, mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, Gramps Morgan, alipost picha ya nyomi la watu wenye mavazi ya kijani na njano na kuandika: “Much love to all our Kenyan fans it was a pleasure to perform and spend time in such a wonderful country next step European tour.”

Gramps

Tatizo la picha hiyo ni kuwa sio ya wapenzi wa muziki wa jijini Nairobi waliohudhuria show yao ya October 3 kwenye viwanja vya KICC, bali ni nyomi la mashabiki wa CCM waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa chama hicho, John Magufuli jijini Mwanza wiki iliyopita.

12135287_161956560818067_886584527_n
Hii ni picha halisi iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii ya CCM

Pamoja na kuwa picha hiyo ni ya Tanzania, wakenya wengi pia wamegundua kuwa Morgan kawaingiza chaka na wengi wamefedheheshwa na kitu hicho.

12105160_1652108418336963_1009929609_n

“This is sad. That’s a picture of a political rally in Tanzania,” ameandika mmoja na mwingine kuandika, “SORRY Gramps Morgan THIS PICTURE IS NOT FROM KENYA..BUT A POLITICAL RALLY IN TANZANIA COUNTRY.”

Mwingine aliandika: We love you Morgan but please this photo isn’t the one! It’s from Tanzania CCM! Crooks.”

Hata hivyo wapo walioingizwa chaka na Gramps kama huyu aliyeandika, “Man look at this crowd in Kenya all to see Morgan Heritage. Astonishing,” huku mwingine akisema, “The Sound system must have been huge for this crowd #impressive.”

Kundi hilo linaundwa na ndugu watano, Peetah Morgan, Una Morgan, Roy “Gramps” Morgan, Nakamyah “Lukes” Morgan na Memmalatel “Mr. Mojo” Morgan bado lipo nchini Kenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents