Mr Nice Kuzindua Album Bilicanas

Mwanamuziki aliyetamba kwa staili ya TAKEU, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ anatarajia kufanya Show ya kuzindua albamu yake ya Tabia Gani katika ukumbi wa Bilicanas.
Mr Nice alisema hii itakuwa mara yake ya kwanza kupanda jukwaani baada ya takribani miaka sita kupita.

Alisema anatarajia kufanya mambo makubwa katika uzinduzi huo, ambao anatarajia kusindikizwa na wasanii kama Aman Temba, Saidi Juma ‘Chege’, Robart Mangwer ‘Ngwea’ na wengine.

Alisema pia atakumbushia nyimbo zake ambazo zilivuma sana kama Fagilia, Kikulacho,Bwana Shamba na nyingine nyingi ambazo zilifanya vizuri.

“Mashabiki wangu natakakuwakumbusha kile ambacho zamani nilikuwa nafanya, narudi
tena kama zamani” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents