Siasa

Msama achukua fomu ya kugombea Spika wa Bunge

MFANYABIASHARA Maarufu nchini Alex Msama leo amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Job Ndugai kujihudhuru.

Baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutangaza kuanza mchakato wa kumsaka mrithi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ambaye alijiuzulu tarehe 6 Januari mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Januari 15, 2022, jijini Dar es Salaam baada ya kuchukua fomu Msama amesema kuwa anauwezo na anaimani na nafasi ya Spika ndo sababu iliyopelekea kuchukua fomu.

“Jambo lolote linapangwa na Mungu nimechukua fomu leo na ninarudisha leo leo, Uongozi unapangwa na Mungu namwachia Mungu na Mamlaka ya Uongozi wa Uchaguzi wafanye maamuzi yao.”

“Uwezo ninao najiamini na nafasi hii Nina iweza kuitumikia leo sitaongea sana kwa kuwa mchakato bado unaendelea namwachia Mungu na Uongozi mzima mchakato uendelee.” amesema Msama

Aidha Katibu wa NEC- Itikadi Uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka alisema mchakato huo wa kumtafuta Spika utaanza kuanzia tarehe 10 hadi 30 Januari mwaka huu.

Amesema hatua hiyo imekuja baada ya Ndugai kuandika barua kwa hiari yake na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM jijini Dodoma.

Amesema kufuatia hilo CCM kinawatangazia wanachama wake wote kwamba utaratibu wa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea atakayechaguliwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujaza nafasi ys Spika wa Bunge.

Ameongeza utaratibu huo ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayotambua Spika kuwa ndio kiongozi mkuu wa Bunge na nafasi hiyo haiwezi kuwa wazi na Bunge likaendelea kufanya shughuli zake.

Akinukuu Katiba hiyo amesema; Ibara ya 84 (i) kutakuwa na Spika ambaye atachaguliwa na wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni wabunge au wenye sifa za kuwa wabunge, atakuwa ndio kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.

“Ibara ya 84(viii) inasema hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge isipokuwa uchaguzi wa spika wakati wowote ambao kiti cha spika kipo wazi.

“Ibara ya 86(i) kimeeleza kutakuwa na uchaguzi wa spika katika kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge jipya, na katika kikao cha kwanza chochote mara baada ya kutokea kiti cha spika kuwa wazi.

“Kwa minajili hiyo, katika kutekeleza matakwa ya kikatiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, nichukue fursa hii kwa niaba ya chama kutangaza kwamba mchakato wa kujaza kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utatekelezwa kwa ratiba ifuatayo sambamba na vikao vya mchujo na uchaguzi wa wabunge wa CCM kabla ya kupelekwa bungeni kuendelea na utaratibu mwingine,” amesema.

Amesema kuanzia tarehe 10 hadi 15 zoezi la kuchukua fomu litaanza rasmi na tarehe 15 ifikapo alasiri zoezi hilo litakuwa limekamilika.

Amesema wale wenye sifa alizotaja wanakaribishwa kuchukua fomu katika makao makuu ya chama ofisi kuu, makao ya chama Dodom, ofisi ndogo Dar au Kisiwandui wakifika watapata maelekezo namna ya kcuhukua fomu hizo.

Amesema tarehe 17 Januri, 2022 Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya Taifa itakutana kwa ajili ya kujadili wagombea na kuishauri Kamati Kuu ya Halmashuri kuu ya Taifa juu ya wagombea ambao wamejitokeza kuomba kiti hicho cha uspika.

“Tarehe 18 hadi 19 Januari kutakuwa na kazi ya kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho ambapo Kamati kuu ya Halmashauri Kuu itafanya kazi hiyo kwa eneo ambalo litaelekezwa.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents