Habari

Msichana mmoja chini ya miaka 15 huolewa kila baada ya sekunde 7 duniani

Msichana mmoja chini ya miaka 15, huolewa kila baada ya sekunde 7, kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Save the Children.

underage-marriage

Utafiti huo umesema kuwa wasichana wenye miaka 10 wanalazimishwa kuolewa na wanaume wenye umri mkubwa katika nchi zikiwemo Afghanistan, Yemen, India na Somalia.

Migogoro, umaskini na matatizo ya kibinadamu, yameonekana kuwa ni chanzo cha kuwaacha wasichana wakiwa hatarini kuolewa wakiwa na umri mdogo.

“Wasichana wanaolewa wakiwa na umri mdogo hawawezi kwenda shule, wana hatari ya kukabiliana na unyanyasaji wa majumbani, kufanyiwa ukatili na kubakwa. Hupata mimba na wanakuwa hatarini kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo HIV,” amesema ofisa mtendaji mkuu wa Save the Children International Helle Thorning-Schmidt.

Ripoti hiyo imepewa jina, Every Last Girl na imekuangikia kwenye siku ya kimataifa ya msichana, Jumanne hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents