Siasa

Mtandao wa Twitter waficha tweets za Trump zinazotishia waandamanaji

Mtandao wa Twitter umeamua kuzificha tweets za Rais wa Marekani Donald Trump zinazotishia kutumia nguvu ili kumaliza maandamano.

Hatua hii imekuwa ni ya kwanza kwa mtandao huo kuficha maudhui ya vitisho kama hivyo hasa kwa kiongozi mkubwa kama Trump.

Kitendo hiko cha Twitter kimefanywa katika maudhui aliyoyaweka Trump kwa kuweka kiunga kinachompeleka msomaji kwenye sera ya maudhui yanayozuiwa katika mtandao huo, ili mtu aweze kusoma ni lazima abonyeze ndipo atakutana na ujumbe huo.
Twitter wamesema kuwa Imeamua kuficha jumbe hizo ambazo zinatishia kundi fulani la watu ambalo linatambulika.

Moja ya Tweet hiyo ilikuwa inasema kuwa “Tutachukua maamuzi magumu kuthibiti lakini tutakapogundua kuna uporaji, hata risasi zitatumika “
Pia, mtandao wa Facebook uliondoa tangazo la Rais Trump lililokuwa na alama ya Utawala wa ‘Nazi’ iliyotumika na wajerumani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents