FahamuHabariSiasa

Mtanzania mmoja afariki Israel kutokana na Vita, Wizara yatoa taarifa

Siku ya leo moja ya habari mbaya kabisa ni hii ya Mtanzania kufariki Israel.. “Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa masikitiko na huzuni imetangaza kifo cha
Clemence Felix Mtenga, Kijana Mtanzania ambaye ni miongoni mwa Watanzania wawili ambao pamoja na raia wa Mataifa mengine walikuwa hawajulikani walipo tangu yaliyopotokea mapigano October 07, 2023 nchini Israel na katika maeneo ya Wapalestina hususani Gaza.

Taarifa iliyotolewa na Wizara haijasema chanzo cha kifo chake na Mji ambao amefia lakini imesema Clemence alikuwa ni miongoni mwa Vijana wa Kitanzania wapatao 260 waliokwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo chini ya Mpango wa Ushirikiano kati ya Serikali ya
Tanzania na Israel.

Tayari Wizara imechukua hatua stahiki ikiwemo
kuijulisha Familia na inaendelea kuwasiliana na
Serikali ya Israel kuhakikisha kwamba taratibu za kurejesha mwili wa marehemu nchini kwa ajili ya
mazishi zinakamilika kwa wakati.

Wizara imesema inaendelea kufuatilia taarifa za
Mtanzania mwingine Joshua Mollel ambaye bado hajulikani alipo tangu yalipotokea mashambulizi hayo
“Wizara inatoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa msiba huu”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents