Habari

Mtengeni Trump – Obama awaasa viongozi wa juu wa chama cha Republican

Rais wa Marekani, Barack Obama amewaasa viongozi wa juu wa chama cha Republican, wajiondoe kumuunga mkono Donald Trump kama mgombea urais wa chama chao.

obama_sotu_2016_ap_img

Kwenye mkutano wa kumpigia kampeni mgombea wa chama cha Democratic, Hillary Clinton, Obama alisema haina maana viongozi hao kupinga kauli za Trump wakati bado wakiendelea kumuunga mkono katika harakati zake za kuingia White House.

Viongozi wengi wa juu wa Republican wamejitenga na Trump baada ya kuvuja kwa video ambayo anasikika akiwadhalilisha wanawake. Alilazimika kuomba radhi.

Obama amesema maneno ya Trump dhidi ya wanawake, yanamnyima hata sifa za kuuza duka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents