Habari
Mto Swakop watiririsha maji bahari kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 11
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2022/02/swakop-river-reaches-ocean-after-more-than-a-decade2022-02-171.jpeg)
Mto Swakop nchini Namibia umemwagika katika Bahari ya Atlantiki kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 11, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha.
Wakiwa na simu mahiri na kamera, watu walikusanyika kwenye mdomo wa mto Jumatano kushuhudia tukio hilo nadra:
Phenomenal… The Swakop River reached the sea this morning for the first time since 2011. Swakopmund residents flocked to the river mouth to witness the great moment.
Video: Contributed pic.twitter.com/RwGgkOXiNy— New Era Newspaper (@NewEraNewspaper) February 16, 2022
Mto Swakop hukauka katika Jangwa la Namib isipokuwa katika misimu ya mvua kali unapotiririka baharini.
Ulitiririka kwa mara ya mwisho katika Atlantiki mnamo Aprili 2011.