Burudani

Muziki wangu ni msafi, sivunji sheria – Roma Mkatoliki

Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki ambaye alikuwa akiuguza majeraha baada ya kutekwa na watu wasiojulikana, amedai anaumizwa na jinsi watu wanavyohusisha tukio hilo na aina ya muziki anaoufanya.

Rapa huyo amedai anaamini anafanya muziki ambao hauvunji sheria za nchi.

“Kwanza niweke sawa, naamini katika muziki ninaofanya na naamini sijafanya kitu kibaya, sivunji sheria na wala siongei maneno mabaya,” Roma alikiambia kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV.

Aliongeza “Naumia sana nikiona mtu anautafsiri vibaya muziki wangu. Mimi sifungamani na upande wowote, hata ukiniuliza kadi ya chama mimi sina kadi ya chama chochote. Kwa sababu nikichukua kadi ya chama chako utasema nimekuwa mwanafamilia wako, wewe ni baba ukikosea nitakunyooshea vipi kidole?. Kwa hiyo napata sana ukakasi nikiona watu Roma wanamtafsiri tofauti, naumia sana.,”

Baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakilihusisha tukio hilo na aina ya muziki wa kuikosoa serikali ambao amekuwa akiufanya.

Jeshi la polisi bado linaendelea na upelelezi wa tukio hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents