Habari

Mvua kubwa yaua watu 20 Kongo

Takribani watu 20 wamekufa katika siku mbili zilizopita katika maporomoko ya ardhi na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hayo yameelezwa jana na mamlaka nchini Kongo. Watu wapatao kumi na tatu hadi sasa wameripotiwa kufariki katika eneo la uchimbaji madini ya dhahabu huko Rubaya, mji wa Masisi huko Kivu Kaskazini.

Jean-Paul Barindikije, katibu wa chama cha wachimbaji madini amesema kuwa walioathirika zaidi ni wachimbaji madini. Polisi wamesema kuwa miongoni mwa watu waliofariki huko Rubaya ni mama mmoja na watoto wake wanne waliosombwa na maji.

Kamanda wa polisi Kambale Muhindo, amesema watu watatu wa familia moja walisombwa na maji ya mto katika eneo la Bihambwe, takribani kilomita 5 kutoka Rubaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents