Burudani

Mwana FA aingia kambini kwenye mazoezi ya masumbwi na nahodha wa timu ya taifa ya mchezo huo

Tunafahamu kuwa licha ya kuwa rapper mwenye mafanikio makubwa, Mwana FA ni msomi wa shahada ya uzamili (masters) katika masuala ya biashara. Lakini si kazi za benki tu ama zinazohusiana na masuala ya biashara anazoweza kuzifanya pale atakapoona muziki umeenza kuzingua.

57d9e1b2cc6b11e2b74c22000a9f1427_7

Apparently Mwana FA can kick some butt!! FA ambaye hivi karibuni ameachia ngoma mpya, ‘Kama Zamani’ yupo busy akijifua na kocha wa masumbwi, Joseph Martin ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya masumbwi Tanzania.

“Work out with Joseph Martin(ex National Boxing Team Captain) was superb today….feeling like Floyd now,yeah,Mr Mayweather,” aliandika FA kwenye picha aliyoiweka kwenye Instagram.

Tutegemee kumuona Mwana FA ulingoni siku za usoni? Bila shaka ni mazoezi ya kujihami tu pale ‘haters’ watakapotaka kumzingua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents