Bongo Movie

Mwana Hery wa filamu ya ‘Pumu’ aachia filamu mpya ‘Mwana Heri’

Msanii mchanga wa filamu Mwana Hery baada ya kufanya vizuri na filamu yake ‘Pumu’ akiwa na King Majuto, ameachia filamu yake mpya iitwayo ‘Mwana Heri’.
Mwana Hery
Mwana Hery

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Mwana Hery amesema filamu hiyo itaonyesha uwezo wake mkubwa wa kuigiza.

“Movie ya ‘Pumu’ niliproduce last year na ndio movie ilionitambulisha, kila mtu ambaye ananijua ananijua kupitia movie ya Pumu. Lakini baada ya hapo nikaja na Makusanya nayo ilifanya vizuri kwa kiasi chake lakini movie yangu mpya Mwana Hery ndio imekuwa gumzo zaidi, movie inauza sana,” alisema Mwana Hery.

Pia muigizaji huyo amewataka mashabiki wa filamu zake kuendelea kusupport kazi zake kwani kuna mambo mazuri yanakuja kutoka kwake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents