Habari

Waziri Mkuu ayakataa madawati ya msaada, ‘huu si wakati wa kupokea vitu vibovu’

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekataa kupokea msaada wa madawati, uliotolewa na Wakala wa Misitu TFS Tanzania.

kassim2

Amegoma kupokea madawati hayo jana alipowasili katika kiwanja cha Mabau, Mtibwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ambapo alikabidhiwa madawati hayo na Meneja wa TFS na kuona hayana kiwango kizuri.

“Ofisa Elimu njoo, kagua haya madawati, yaliyo mazuri nitayapokea na yaliyobaki yasiyo na ubora yarudishwe haraka sana yakatengenezwe upya, huu si wakati wa kupokea vitu vibovu”, alisema.

Hata hivyo baada ya Ofisa Elimu (Msingi) wa Wilaya ya Mvomero, Michael Ligola kukagua madawati 102 yaliyoletwa uwanjani hapo, madawati 84 yalibainika kuwa ni mabovu na 14 tu ndiyo yalikuwa mazima.

Alisema, “natambua dhamira ya TFS ya kuunga mkono jitihada za serikali za kumaliza tatizo la upungufu wa madawati, lakini hawezi kupokea madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango”, alisema Waziri mkuu.

Pia aliwasisitiza wazazi na walezi wa wilaya hiyo, kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Serikali imewapunguzia mzigo kwa kuwaondolea michango na ada, hivyo tumieni fursa hiyo kwa kuwapeleka shule watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule na wasimamie masomo yao,” alisema.

CHANZO: HABARI LEO

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents