Habari

Mwanamke aliyevua hijab hadharani atupwa jela miaka miwili

Mwanamke mmoja mjini Tehran nchini Iran amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kuvua hijab mbele ya watu wengi.

Wakili wa mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Abbas Jafari Dolatabadi, amesema kuwa mteja wake alivua hijab hiyo kwa lengo la kuishinikiza serikali nchini humo kuwachukulia hatua viongozi wanaokamatwa kwa vitendo vya rushwa.

Akihojiwa na Shirika la Habari la Tasnim, Dolatabadi amesema licha ya kumpigania mteja wake mahakama nchini humo imemuhukumu mwanamke huyo miezi 24 jela.

Dolatabadi, amesema kuwa licha ya hukumu hiyo tayari ameshapeleka maombi ya kukata rufaa juu ya adhabu hiyo.

Gazeti la Daily Mail limeeleza kuwa zaidi ya wanawake 30 nchini Iran kwa mwaka 2018 wamefungwa jela kwa vitendo vya kuandamana kwa kuvua hijab, ambapo ni kosa kisheria nchini humo.

Kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, mwanamke atakayeonesha nywele zake hadharani hufungwa kifungo cha zaidi ya miezi miwili au kupigwa faini ya dola $25 sawa na tsh 56,000/=

Jeshi la polisi nchini Iran kufuatia ongezeko la matukio hayo limetangaza kuwa kwa mwanamke yeyote nchini humo atakayeandamana kwa kuvua hijab atachukuliwa kali huku bunge likitaka adhabu iongezwe hadi miaka 10.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents