Siasa

Mzee wa Upako awaonya wana siasa na kumtabiri rais ajayo “Amani ni muhimu kuliko chochote, fuateni haki lindeni amani yetu” (+Video)

Mchungaji wa kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako, amefunguka na kuwaomba wana Siasa nchini kudumisha amani ya nchi yetu kwa kutokujali maslahi yao binafsi na badala yake waangalie maslahi ya taifa kwa ujumla.

Mzee wa Upako amewaasa vijana wasije kushawishiwa na mtu kufanya fujo kipindi cha uchaguzi kwani ataharibu ndoto zake za maisha na huenda akasababisha ulemavu kwa mtu ambaye hatajali maisha yake.

Mzee wa Upako amemtabiri Rais ajayo kuwa anasifa za kuwajali wananchi wake na kusema Rais ajayo ni yule aliyejali maisha ya Watanzania kipindi cha Corona maana hakusikiliza maneno ya watu wenye pesa zao nje ya nchi bali aliangalia maisha ya mtu wa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents