HabariMichezo

Nahodha haruhusiwi kuvaa beji ya ‘One Love’ Qatar

Ni marufuku kwa manahodha wa timu za taifa kuvaa beji (badge) za ‘One Love’ ambazo zina hashiria mapenzi ya jinsia moja kwenye michuano ya Kombe la Dunia Qatar na kukiuka hilo mchezaji huyo atakumbana rungu la FIFA kwa kukiuka sheria za vifaa za FIFA.

Manahodha kutoka mataifa tisa (9) Barani Ulaya akiwemo staa wa Uingereza Harry Kane, Gareth Bale wa Wales na Manuel Neuer kutoka Ujerumaniwalipanga kuvaa kitambaa cha ‘One Love’ kinachohusishwa na mapenzi ya jinsia moja katika michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Qatar nchi ambayo inaharamisha uhusiano wa watu wa jinsia moja.

Kwa mujibu wa Bild, Chama cha soka Ujerumana kinafikiria kama nahodha wao, Neuer anaweza kuvaa kitambaa hicho, wakati Harry Kane yeye akitarajiwa kuvaa siku atakapowakabili Iran leo siku ya Jumatatu.

Kuvaa nguo zisizo rasmi kama beji hiyo itapelekea kwa mchezaji kupewa adhabu ya faini ama kupata kadi za njano. Mtendaji Mkuu wa FA, Mark Bullingham amesema kuwa Uingereza ipo tayari kwa kupigwa faini kwa kuvaa kitambaa hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents