Burudani

Nandy alamba deal la mamilioni ya pesa ‘uongozi wangu umenipambania’ (Video)

Msanii wa muziki Nandy ametangazwa na kampuni ya simu, Halotel kuwa balozi wao mpya kupiti promotion yao mpya ulioizindua uitwayo, Ninogesha.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba na msanii huyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema kampuni imemchagua Nandi kwa sababu ana uwezo wa kuwa na mchango chanya utakaosaidia kukuza mauzo ya bidhaa na huduma, pamoja na kuimarisha jina la kampuni.

“Nandy ni msanii anayekonga nyoyo za mashabiki wake kupitia wimbo wake unaovuma kwa jina la ‘Ninogeshe’ na kumpa umaarufu unamfanya afahamike kwa watu wa rika zote. Unampa umaarufu ambao utasaidia kuiwakilisha vema kampuni ya Halotel,” alisema Semwenda.

Kwa upande wake, msanii wa bongofleva, Faustina Mfinanga (Nandy) amesema hiyo ni fursa kubwa na ya kipekee kwake kuwa miongoni mwa familia ya kampuni hiyo na kupewa jukumu la kuiwakilisha ipasavyo kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla kutokana na huduma bora za mawasiliano inazotoa.Huduma ya Halopesa inatolewa na zaidi ya mawakala 55,000 wanawahudumia zaidi ya wateja milioni 1.5 walioenea nchi nzima.

Msanii chipukizi wa kike wa nyimbo za kizazi kipya (bongo fleva), Faustina Mfinanaga maarufu kama “Nandi” akizungumza na waandishi wa Habari uzinduzi wa Kampeni mpya iitwayo “NINOGESHE NA HALOPESA” itakayo wawezesha wateja wa mtandao wa Halotel Kutuma pesa bure kupitia Huduma ya Halopesa huku wakipata muda wa maongezi wa bure kila wanapoweka pesa kupitia kwa mawakala walioenea nchi nzima. Nandi ndio Balozi wa Kampeni Hii ya Halopesa.

Related Articles

2 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents