Burudani

Napenda kufika sehemu fulani lakini nashukuru kuwa hapa – Belle 9

Staa wa muziki wa R&B Belle 9 amesema bado ana safari ndefu kufika sehemu anayohitaji katika muziki wake.
Belle 9

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo wa ‘BurgerMovieSelfie’ ameiambia Bongo5 kuwa anaamini kila kitu kinakuja kutokana na juhudi za mtu binafsi.

“Management ni kitu muhimu sana lakini kama kuna bidii kubwa, moyo wa kazi, passion ya kitu ambacho unafanya,” alisema Belle.

“Kusema ningepata management mapema ningekuwa mbali zaidi nitakuwa napingana na mungu, kama tumeanza na management na tumeanza kupata haya, tutarajie makubwa zaidi. Kila mtu ana ndoto ya kufika huko, hakuna mtu anaweza kukwambia position aliyopo ndio mwisho wake, binafsi napenda kufika sehemu fulani lakini nashukuru kuwa hapa,” aliongeza Belle 9.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents