Burudani

Nay adai hela pamoja na mali anazomiliki zina thamani ya bilioni 1

Staa wa muziki Nay wa Mitego amedai kuwa hela anazomiliki benki pamoja na mali anazomiliki zina thamani ya bilioni 1.
nay
Nay akiwa kashika mabunda ya pesa

Akizungumza katika kipindi cha Weekend Chat Show cha Clouds TV Ijumaa hii, Nay alisema biashara pamoja na muziki wake ni vitu vinavyomwingizia pesa nyingi.

“Mimi mali zangu na kila kitu zinafika kwenye bilioni hivi, ukichanganya hela zilizo benki pamoja na biashara ninazofanya thamani yake zinafikia bilioni moja na kitu. Sitaki kudanganya watu sijui kwenye bilioni 2 huko,” alisema Nay.
IMG_0510
Mojo kati ya gari zake

Nay alisema hela hizo amezipata kupitia biashara ya daladala pamoja na muziki wake.

Rapa huyo mwaka 2014 alihamia kwenye nyumba yake iliyopo Mbezi jijini Dar na kudai nyumba hiyo ina thamani ya milioni 200.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents