Technology
Netflix sasa inapatikana Afrika nzima
Kampuni maarufu ya kutazama TV, filamu na series mtandaoni, Netflix imeongeza wigo wake kwa kuzifikia nchini 130 sasa zikiwemo zile za chini ya jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania.
Kampuni hiyo ya California sasa imeingia kwenye nchi zote 54 za Afrika. Mteja atalipa dola $7.99 kwa mwezi kuangalia chochote atakacho.
Kama kutakuwepo internet yenye speed ya uhakika Netflix itavutia wateja wengi wa Tanzania.
Netflix pia imekuja kwenye kipindi ambacho gharama za kulipia DSTV yenye channel nyingi zaidi zikiwa zimepanda.