Mitindo

Ni Wema na Lulu tayari Jumsuit hii

Hello hello wasomaji wetu wa Bongo5 habari, leo tunakutana tena katika ulimwengu wa mitindo na kama ilivyo ada yetu kupeana habari na dondo za mitindo zinazofanya vizuri. Na ndio maana leo tunaitazama Jumsuit mpya mjini inayobamba poa.

Nguo hii mpaka sasa imeonekana kuvaliwa na mastaa wawili wa filamu Bongo yaani Wema Sepetu ambaye alivaa katika Instagram Party iliyofanyika nchini Rwanda na hivi karibuni akatinga tena Jumsuit kama hiyo katika mitoko yake.



Ila muigizaji Elizabeth Michael’ Lulu’ alitinga kwa mara ya kwanza Jumsuit hiyo katika uzindunzi wa tuzo za filamu zilizoandaliwa na kituo cha Azam na alipendeza kweli kweli.

Huwenda Jumsuit hizi zimevaliwa pia na mastaa wengine hapa Bongo na nje ya Bongo sema tu! hatuja bahatika kupata picha zao.

Aina hii ya nguo iliyounganisha blauzi na suruali inakuwa na rangi tofauti tofauti kama njano,maua maua yenye mchanganyika wa pinki,zamabara na rangi zingine zinaonganishwa na suruali ya bwanga nyeusi ambalo hutoa nafasi hata kwa wenye miili mikubwa kuvaa.

Je! wewe kama mdau wa mitindo una jumsuit gani mpaka sasa kabatini kwako?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents