Burudani

Nicki Minaj awafyekelea mbali Cardi B,Drake,Migos,Dua Lipa na wengine MTVEMA atwaa tuzo mbili , awashukuru mashabiki zake (+Video)

Nicki Minaj awafyekelea mbali Cardi B,Drake,Migos,Dua Lipa na wengine MTVEMA atwaa tuzo mbili , awashukuru mashabiki zake (+Video)

Rapper wa kike kutoka nchini Marekani Onika Tanya Maraj kwa jina la kisanii Nicki Minaj amefanikiwa kutwaa tuzo mbili usiku wa kuamkia leo nchini Uhispani. Nicki amefanikwa kushinda tuzo hizo kwa kuwabwaga wasanii wakubwa kama akina Drake,Cardi B,Migos,Dua Lipa,na Post Malone.

Katika vipengele hivyo alivyofanikiwa kushinda moja ya kipengele alikuwa pamoja na mpinzani wake mkubwa kwa sasa mwanadada Belcalis Marlenis Almánzar kwa jina maarufu Cardi B, ambacho kilijulikana kama  ‘Best Look’ Katika Category hiyo mwanadada Nicki Minaj alikua anachuana na Cardi B, Dua Lipa, Migos na Post Malone.

Lakini pia katika kingine ambacho Nicki Minaj amefanikiwa kushinda ni  ‘Best Hip Hop’ ambacho alichuana na wasanii kama:- Drake, Eminem, Migos na Traviss Scott.

Baada ya kunyakua tuzo hizo mbili Nicki aliweza kupafomu jukwaani pia kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweza kuwashukuru mashabiki zake waliofanikiwa kumpigia kura kwa kusema haya:-

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents