Habari

NIDA yatakiwa kuongeza ‘spidi’ ya kusajili watumishi wa serikali

Serikali imeitaka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (Nida) kuhakikisha wanasajili mtumishi yeyote hata kama hana vyeti ndani ya siku 14. Mhusika huyo anatakiwa arejeshe vyeti vyake kwa ofisa utumishi.

kairuki

Waziri wa nchi, ofisi ya rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, Angella Kairuki alisema hayo katika ziara yake ya siku moja mkoani Mwanza ambapo alitembelea wilaya za Nyamagana, Misungwi na Ilemela.

Alisema kila mtumishi wa umma anatakiwa kuhakikisha kuwa anapata Litambulisho cha taifa kabla ya Disemba mwaka huu na kuwashukuru wale wote waliojitokeza mpaka sasa kwa ajili ya suala hilo.

“Ni lazima kila mtu apate kitambulisho cha taifa lakini kwa sasa tumeanza na watumishi wa umma kisha baadaye watafuata watu wote,”alisema Kairuki.

Aidha Kairuki ameipongeza Nida kwa juhudi za kuendelea kusajili watumishi wa umma katika kuhakikisha wanapata vitambulisho vya taifa, huku akiahidi kuongeza mashine za kutosha kwaajili ya usajili wa vitambulisho hivyo.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents