Burudani

Nikki Mbishi azungumzia kuongoza kwa downloads nyingi kwenye website ya mdundo ya Kenya

Kwa mujibu wa ripoti ya malipo ya robo ya kwanza mwaka 2014 ya mtandao wa kupakua muziki wa Kenya, mdundo.com, Nikki Mbishi ndiye aliyeongoza kwa downloads nyingi.

eOMgYyhu

“Tanzanian hip hop heavy weight Nikki Mbishi leading the pack in returns with over 7,000 downloads in total yet he has little over 2 months since he signed up with Kenya’s leading download platform Mdundo,” umeandika mtandao huo.

Nikki Mbishi ameiambia Bongo5 kuwa hiyo ni habari njema kwake na inampa picha ya jinsi gani muziki wake unakubalika si tu Tanzania bali Kenya pia.

“Kitu ninachojua ni kwamba mbali na hizo downloads na kila kitu, nimegundua kwamba Kenya nina watu wangu wengi wanaosupport kazi yangu. Moja kwa moja najua muziki wangu kule (Kenya) una nafasi kubwa sana,” amesema Nikki.

Rapper huyo wa ‘Nay wa Mitego’ amesema hata mixtape yake imefanya vizuri zaidi mwaka jana.

“Ndio mixtape inayofanya vizuri na bora kuliko zote zilizotoka kwa mwaka huo ulioisha. Kama kufanya vizuri pia inawezekana ilianzia ndani kabla ya nje ingawa bado pia itanijenga kwamba nahitaji nifanya kitu kizuri zaidi,”

Msikilize hapo chini.

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/129802232″ params=”color=ff6600&auto_play=false&show_artwork=true” width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents