Burudani

Nimeshindwa lakini bado sijaikatia tamaa siasa – Keisha

Keisha ni mmoja wa wasanii walioshindwa kupitia kwenye kura za kuwapata wabunge wa viti maalum kupitia CCM lakini amesema hajakata tamaa.

keisha

Keisha ameiambia Bongo5 kuwa ingawa alishinda katika kura za maoni, katika kura za taifa aliibuka katika nafasi ya nne.

“Zile za kwanza zilikuwa ni kura za maoni nilishinda, then kulikuwa na kura za kitaifa ambapo nilikuwa mtu wa 4 katika watu 18,” alisema.

“Watu wanaotakiwa ni wawili, kwahiyo wawili ndio walioshida katika upande wa walemavu. Basi maisha yanaendelea na tunaendelea na kampeni kwa sababu ni chama changu. Lakini hii hatua niliyofikia imenijenga kwa sababu wakati nashiriki, sikutengemea ushindi peke yake, nilijua pia kuna kushindwa kwa sababu kuna watu walianza hiyo safari muda mrefu. Kama hao walioshinda wawili walianzia mwaka 2010, kwahiyo mtu asiyekubali kushindwa siyo mshindani.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents