Burudani

Nisher: Sasa hivi nina mchumba na mwakani natarajia kuwa baba

Muongozaji wa video nchini , Nisher David George maarufu kama Nisher ameweka wazi kuwa mchumba wake ambaye ameanza kumuweka hadharani hivi karibuni ni mjamzito.

nisher na mchumba-4

Nisher ameiambia Bongo5 kuwa ‘baby’ wake aitwaye Sandra ni mjamzito wa mwezi mmoja na nusu hivyo wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza mwakani 2016.

nisher na mchumba-5

Ukitembelea akaunti za mitandao ya kijamii za Nisher na mrembo huyo utagundua ‘love is in the air’, kutokana na wote kupost picha nyingi za pamoja kitu ambacho zamani Nisher alikuwa hafanyi.

Nini kimemsukuma Nisher kuamua kumuweka wazi mpenzi wake? Najua cha kwanza ni kwasababu ni mrembo (LOL), cha pili …“Niliona niweke kilakitu wazi kutokana na ilifika time nikaona nahitaji kukua, na kuachana na mambo ya ujana na kua mtu mzima, pia kuepuka usumbufu.” Alisema Nisher.

nisher na mchumba-2

Je huyu ni moja ya warembo ambao Nisher amekutana nao wakati wa kutafuta video vixens? Hakusita kutuambia walivyokutana;

“Long story short, tumefahamiana before, Sema hatukua serious kivile, ila tulikua washkaji tu… Sema there’s something about here iliyoniteka kuliko Mwanamke yeyote mwingine!!.”

Kuhusu ndoa Nisher amesema “Ndoa eventually ntafunga, ila hakuna haraka!”

nisher na mchumba-9

nisher na mchumba-11

nisher na mchumba-1

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents