Burudani

Nitabaki kuwa mfalme – Alikiba

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba amesema atabaki kuwa mfalme wa muziki hapa Bongo ingawaje anaandamwa na watu aliokataa kuwataja moja moja.

Alikiba

Akitumia lugha ya mafumbo, Alikiba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameoneshwa kukerwa na jambo hilo na kuamua kutema cheche huku akihoji kama walimpa kitanda basi waje wamtandikie alale kabisa.

“The KING ll always Be a KING. je Umeshakitandika nilale MALKIA wangu wa nguvu ??”,ameandika Alikiba pasi kujua ujumbe huo umemulenga nani.

Jana Tarehe 21 Agosti, Rapa Fid Q aliachia remix ya wimbo wake ‘Fresh’ ambao amewashirikisha Diamond Patnumz na Rayvanny, wimbo ambao mashairi ya Diamond yameonekana kuleta utata huku watu wengi wakihusisha kumlenga Alikiba.

SOMA ZAIDI- Alikiba aanza kutema cheche za Kipusa ‘they call me a heartbreaker?’

Moja ya mashairi hayo Diamond anasema “Ukinichukia sikosi hela hivyo kwangu sio kesi, Kunicompare na Cinderella haiwezi kuwa fresh” hapa swali linakuja Cindeella ni nani? bila shaka wote mnafahamu wimbo WA Cinderella uliomtoa Alikiba kwenye game.

SOMA ZAIDI-Makala: Alikiba ukishindwa kujifunza kwa Davido jifunze hata kwa Aslay

Na mashairi mengine ambayo yanahusishwa moja kwa moja na posti ya Alikiba ni pale Diamond Platnumz alivyosema “Si walitaka kiti, nimewapa hadi kitanda wakalale” kwani Alikiba nae ameonekana kukerwa na mistari hiyo na kujibu “je Umeshakitandika nilale MALKIA wangu wa nguvu?”.

Usikilize hapa chini wimbo wa Fid Q aliowashirikisha Diamond Platnumz na Rayvanny ‘Fresh Remix’

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents