Michezo

Nyota hawa 20 wa Yanga SC kuelekea Shelisheli kesho tayari kuivaa St Louis, Chirwa ‘Out’

KIKOSI cha Yanga Sc kinatarajia kusafiri kesho asubuhi kueleka Shelisheli tayari kwa mchezo wa marejeano na wenyeji  St Louis Fc kwenye ligi ya mabingwa afrika mchezo ulipangwa  kuchezwa Jumatano ijayo Stade Liete.

Muda mfupi  uliopita  Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa jumla ya nyota 20 na viongozi 10 kati yao nane kutoka benchi la ufundi watasafiri asubuhi ya kesho  kupitia Nairobi tayari kwa mchezo huo muhimu  siku ya Jumatano.

Maandalizi yote muhimu yamekwisha fanyika, timu imefanya mazoezi ya mwisho leo tayari kwa safari hiyo. Kwenye kikosi nyota waliyokuwa na majeraha ya muda mrefu kama Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Abdallah Shaibu na Yohana Mkomola wataendelea kukosekana hii ni kwa sababu bado wanauguza majeraha,kucheza ugenini  kunachangamoto zake lakini tumejiandaa vizuri kwa sababu tushacheza nje mara nyingi hivyo hakuna hofu kati yetu.

Akiendelea zaidi Ten amesema kuwa, mchezaji Thabani Kamusoko ambaye amepona majeraha yake hivi karibuni na kuanza mazoezi mepesi,ameondolewa kutoka orodha ya nyota ambao wangesafiri kueleka Shelisheli ili apate muda wa kujifua zaidi na kurejesha makali yake, mchezaji Obrey Chirwa  pia hayumo kwenye orodha hiyo kwa sababu ya maumivu ya misuli.

Ilikuwa asafiri kuelekea Shelisheli, lakini imekazimu benchi la ufundi kumuondoa kwa sababu bado hajawa sawa asilimia 100, anahitaji muda wa kujifua zaidi ili kupata utimamu wa mwili tayari kwa mapambano uwanjani , daktari wake pia amethibitisha kuwa mchezaji anatakiwa apate muda wa kujiweka sawa kabla hajaanza kucheza mechi kulingana na majeraha aliyokuwa nayo.

Orodha kamili ya wachezaji ambao safiri kuelekea Shelishelini kama Ifuatavyo:

Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya, Youthe Rostand, Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Gadiel Michael, Nadir Hariub, Patto Ngonyani, Kelvin Yondani, Said Juma, Papy Tshishimbi,Pius Buswita, Raphael Daud, Yussuf Mhilu, Ibrahim Ajib, Said Mussa, Emmanuel Martin, Godffrey Mwashiuya, Juma Mahadhi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents