Habari

Ofisi ya Hakimiliki yatoa somo kwa Viongozi wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho

Akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare aliwasisitiza wadau hao kuzingatia suala la mikataba wanayosaini wanapofanya shughuli zao.

“Hapa mko makundi mbalimbali lakini ni vyema mfahamu wajibu
wenu kila mmoja katika kunufaika na kazi zenu katika muktadha wa
hakimiliki mfano kwenu wachezaji wa sarakasi ni vyema mnapoenda
kwenye maonesho katika matamasha muweke vizuri mikataba yenu katika maudhui yatakayorekediwa matumizi yake baada ya tamasha ili kama video hizo zitatumika kurushwa tena katika televisheni au katika matangazo basi muweze kunufaika na mapato yake,’alisema
Doreen.

Pamoja na hayo nae Afisa Sheria Ofisi ya Hakimiliki Zephania
Lyamuya alieleza kuwa katika uanzishwaji wa Kampuni za
kukusanya Mirabaha na kugawa wadau wenyewe ndiyo watahitajika
kupanga viwango vya kulipwa kwa maeneo yanayotumia kazi hizo.

“Kitengo cha Sheria katika Ofisi ya Hakimiliki kinajukumu la kisheria
la kusuluhisha migogoro ya hakimiliki na kutoa ushauri wa
kisheria”’alisema Lyamuya.

Nae Meneja wa Usajili na Kumbukumbu Philemon Kilaka katika wasilisho lake la hakimiliki na umuhimu wa kusajili kazi aliwasihi wadau hao kusajili bunifu zao ambapo alifafanua kuhusu haki mbalimbali katika hakimiliki ambazo ni haki za uchumi na haki za kimaadili.

Halikadhalika Afisa Hakimiliki Mwandamizi Naomi Mungure alieleza kuhusu mikakati ya Ofisi katika kupambana na uharamia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents