Habari

Mgumba awasimamisha kazi watumishi 21 Tanga

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amewasimamisha kazi watumishi 21 mkoani humo kwa tuhuma za kuhusika na hujuma katika tukio la moto lililochoma ghala la kuhifadhi bidhaa za magendo kwenye bandari ya Tanga mwezi Oktoba mwaka huu.

21 wasimamishwa kazi tukio la kuungua ghala

Mgumba amefikia uamuzi huo baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi kuhusu tukio hilo kutoka kwa kamati ya kuchunguza tukio hilo aliyoiunda Ili kuchunguza chanzo cha moto huo.

Amesema watumishi hao wamesimamishwa kazi Ili kupisha uchunguzi kutokana na kuitia hasara serikali baada ya tukio hilo la kuungua moto ghala la kuhifadhia bidhaa za magendo kwenye bandari ya Tanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents