Burudani

P THE MC: Haikuwa rahisi mwanzoni kupata collabo na wasanii wasio wa rap

Rapper P The MC amesema mwanzoni wakati anachukuliwa kama rapper wa hip hop ngumu haikuwa rahisi kupata collabo na wasanii tofauti na style yake.

12070787_239583199728755_943615895_n

P ni miongoni mwa mamcee waliopata umaarufu kupitia Kilinge cha Tamaduni Muzik.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, P amedai kuwa tangu atoe wimbo wake Na Mimi aliomshirikisha Jux mambo yamebadilika.

Na Mimi ni wimbo uliotayarishwa na Dully Sykes kwenye studio zake za 4.12. Kuna uwezekano mkubwa rapper huyo akawa kwenye orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye Fiesta ya mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents