Burudani

Padri aliyesimamishwa kazi kwa kosa la kutumia muziki wa Hip Hop kanisani amtaja Diamond Platnumz (+video)

Padri aliyejipatia umaarufu nchini Kenya kwa kutumia muziki wa Hip Hop kanisani ili kushawishi vijana kuhudhuria kwenye Ibada, Paul Ogalo amefunguka kuwa ana uwezo mkubwa wa kuimba kila aina ya muziki na yupo tayari kufanya kolabo na msanii yeyote akiwemo Diamond Platnumz.

Fr. Paul Ogalo

Padri Ogalo kupitia mahojiano yake na BBC amesema kuwa anauwezo wa kufanya kolabo na wasanii wakubwa nchini Kenya kama Nameless, Willy Paul, Size 8, Wyre na kwenda mbali zaidi kwa kumtaja Diamond Platnumz.

Naweza kufanya kolabo na watu kama Willy Paul, Wyre, Size 8, Nameless na wengine hata Diamond Platnumz,“amesema Padri Ogalo.

Jana Kanisa Katoliki nchini Kenya kupitia kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Homa Bay,  Philip Anyolo lilitangaza kumsimamisha kazi Padri huyo kwa mwaka mmoja kwa kitendo cha ku-rap kanisani. Tazama mahojiano yake na BBC hapa chini

https://youtu.be/FZtrtKfBG9I

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents