Bongo Movie

Patrick Kanumba kurejea katika filamu mwakani

Msanii wa filamu, Othman Njaidi a.k.a Patrick Kanumba ambaye ni zao la marehemu Steven Kanumba amefunguka ujio wake katika tasnia hiyo.

Patrick amesema mwakani anatarajia kurejea katika filamu baada ya kujikita katika masomo kwa kipindi kirefu na kazi tayari zimeshafanyika.

“Mpaka sasa nipo kimya ila soon inshallah Mungu akifanya wepesi tunaanza mwakani rasmi upya, nilikuwa nasoma na bado mimi ni wanafunzi,” Patrick ameiambia Bongo5.

Katika hatua nyingine amesema kuna uwezekano wa kuja kufanya tena kazi na Jennifer ambaye waliigiza wote movie ya Uncle JJ na marehemu Kanumba.

“Zipo nyingi sana kama tulivyokuwa shule kazi nyingi zinakuwa zinajitokeza sema kwa sababu tuliamua tujikite kwanza kwenye masomo, kwa hiyo kazi nyingine tukawa tunaziacha na tunashuru Mungu waliokuwa wanataka kutupa kazi walikuwa wanatuelewa” amesisitiza Patrick.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents