Burudani

Paul Okoye azilaumu media za Naija kwa kuukuza ugomvi wao, ‘never underestimate the power of blood’

Baada ya mapacha wa P-Square na kaka yao Jude Okoye kuthibitisha amani imerejea baina yao, Paul Okoye amezitupia lawama media za Nigeria kuwa zilikuza ugomvi wao ambao amedai ulikuwa mdogo na wa kawaida.

p-square na wake zao

“Ugomvi na mgogoro wa mapacha sio kitu kikubwa ni vile tu Naija media waliukuza kupita kiasi” alisema Paul.

Paul pia amemtetea mke wa pacha wake Peter kuwa hakuhusika kwa lolote katika mgogoro wao hivyo kuwaomba watu wasimlaumu Lola sababu hana hatia.

Paul aliongeza kuwa watu wasichukulie poa nguvu ya damu (ndugu) kwa kumaanisha kuwa sio kitu rahisi kuwatenganisha.

Hiki ndicho alichokiandika Paul Okoye kupitia ukurasa wake wa facebook jana:

Please whatever happen was not cause by any woman, pls and pls stop blaming ma brother’s wife Lola for wat she’s innocent. Twins fight and quarrel is not a big deal only dat naija media over-emphasized it, but never underestimate the power of blood. It’s thicker than water. Much love to y’all. #Family #ForeverPsquare

paul

Wakati huo huo siku moja baada ya ndugu hao kuthibitisha kuwa wameyamaliza matatizo yao, Peter, Paul na Jude Okoye walionekana pamoja juzi katika sherehe ya model aitwaye Sarah Ofili.

p1

p2

p3

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents