Bongo Movie

Pengo la marehemu Kanumba litazibika tu – Gabo Zigamba

Msanii wa filamu anayefanya vizuri na filamu ‘Safari ya Gwalu’ Salim Ahmed aka Gabo Zigamba amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wa filamu wakiwa na juhudi wanaweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba.
14291912_663339300495519_6955797915967746303_n
Gabo Zigamba

Mwigizaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa filamu ambao wanafanya vizuri kwa sasa, amedai kama wasanii wakiamua kufanya kazi kwa bidii basi kila kitu kinawezekana.

“Pengo la marehemu Kanumba litazibika tu ingawa najua tobo la panya huwezi kuziba na mkate ila tutajitahidi kuziba,” Gabo alimjibu shabiki katika Kikaango cha EATV.

Aliongea,”Niwashauri watu wawe makini kwenye nidhamu, wawe makini kwenye elimu na pia wasikate tamaa katika mambo wanayofanya”

Mwigizaji huyo amemtaja Single Mtambalike kuwa ndiye mwigizaji wake bora kwa sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents