Mitindo

Picha: Blackfox Models Africa yatua Mwanza kwa kishindo

Kampuni ya Blackfox Models Africa ya jijini Dar es salaam weekend hii ilitua jijini Mwanza kwaajili ya kutafuta models wapya pamoja na kufungua ofisi mpya ya kampuni hiyo.

Models wakiandikishwa

Models mbalimbali wa mkoa huo walipata fursa ya kuonyesha vipaji mbalimbali mbele ya timu nzima ya Black Fox.

Akiongaea na Bongo5 wiki hii Mkurugenzi wa kampuni ya Black Fox Africa,  Aj Mynah amesema wamefanikiwa kuwapata vijana 15 ambao watakuwa wanawatumia katika shughuli zao mbalimbali za Modeling.

“Tumefanya casting ya vijana wapya wa Black Fox kwa upande wa kanda ya ziwa Mwanza kwaajili ya ofisi yetu mpya ya huku. Kwa hiyo tunawashukuru sana Gold Crest Hotel walitupatia ukumbi, pia tunawashukuru Lake FM pamoja na Genic studio kwa mambo mazuri waliotufanyia,” alisema Aj.

Aj amesema malengo ya kampuni hiyo ni kufungua matawi nchi mzima pamoja na Afrika. Angalia picha.

Mkurugenzi wa kampuni ya Black Fox Africa, Aj Mynah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents