Habari

Picha: Kesi ya Halima Mdee yapigwa tena kalenda

Kesi ya kutoa lugha chafu inayo mkabili Mbunge wa Kawe,Halima Mdee imeahirishwa mpaka September 12 mwaka huu, kutokana na upelelezi kutokamilika.

Halima mdee anatuhumiwa kutoa lugha Chafu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano wake katika Baraza la Wanawake Chadema(BAVICHA).

Mawakili wa Halima Mdee, wakiongozwa na Wakili Hekima Mwesigwa wamewasilisha pingamizi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa. Ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe tajwa hapo juu.

Hata hivyo Halima Mdee, alikamatwa Julai 4 2017 na Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni Dar es salaam kwa agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi.

Picha: Salum Kaorata

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents