Michezo
Picha: Mmiliki wa Leicester, Aiyawatt atua kuangalia mazoezi kwa Helkopta
Mwenyekiti na mmiliki wa klabu ya Leicester, Aiyawatt Srivaddhanaprabha ametua katika mazoezi ya timu hiyo akitumia usafiri wa helkopta.
Mwenyekiti huyo raia wa Thailand alifika mazoezi na kushuhudia vijana wake wanavyojifua kabla ya kufanya mazungumzo mafupi na Kocha Claudio Ranieri.
Leicester kwasasa wako kileleni wakiwa na pointi 72, wakifuatiwa na Tottenham yenye pointi 65 huku Arsenal katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 59.
Leicester ikiwa inaenda ukingoni mwa Ligi Kuu ina matumaini makubwa ya kubeba ubingwa,